Shabaha
- Kueleza maana ya ala za sauti.
- Kutaja aina mbili kuu za ala za sauti.
- Kueleza tofauti kati ya aina mbili kuu za ala za sauti.
- Kutoa mifano sahihi ya kila aina kuu ya ala za sauti.
Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
Kudurusu
Sauti ni mlio unaotokana na tamko. Ni kipashio kidogo zaidi cha lugha kisicho na maana.
Maagizo
Kwa kutumia ubunifu na maneno yako mwenyewe, andika maelezo mafupi juu ya somo hili kwenye kitabu chako cha mazoezi unapoendelea kusoma na kisha uwasilishe maelezo yako kwa mwalimu wako wa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha uhakiki na maoni yanayofaa.
Msamiati
Ala: Instrument
Ainisha: Classify
Jumuisha: Include/Comprise
Kidogo: Small
Kipashio: Piece/Element
Kundi: Group
Lugha: Language
Shughuli: Activity
Sogea: Move
Tamka: Pronounce
Viungo: Parts.
Shughuli 1: Maana ya ala za sauti
Kutamka ni kule kutoa kwa sauti za maneno ya lugha fulani kinywani.
Ala za sauti ni viungo vya mwili ambavyo vinatumiwa kutamkia sauti.
Picha ifuatayo inaonyesha ala mbali mbali za sauti.


Kumbuka: Midomo ni miwili (mdomo wa juu, na mdomo wa chini).
Shughuli 2: Aina kuu za ala za sauti
Ala za sauti zinaweza kuanishwa katika makundi mawili yafuatayo:
- ala sogezi
- ala tuli.
Shughuli 3: Ala sogezi
Kundi hili linajumuisha viungo vya kutamkia ambavyo husogeasogea wakati sauti inapotamkwa.

Midomo

Ulimi
Shughuli 4: Ala tuli
Kundi hili linajumuisha viungo vya kutamkia ambavyo havisogeisogei wakati sauti inapotamkwa.
Mifano ya ala tuli
Kaakaa gumu
Kaakaa laini
Fizi
Meno
Shughuli 5: Wimbo kuhusu ala za sauti.
Kariri wimbo ufuatao ili kukusaidia kukumbuka kwa urahisi ala tofauti za sauti.
ALA ZA SAUTI
Umio wa hewa
Nyuzi za sauti
Chemba cha kinywa
Chemba cha pua
Kidakatonge
Kaakaa laini
Ulimi, Pua
Kaakaa gumu
Ufizi, Meno
na Midomo
ni Ala Za Sauti.