Shabaha
- Kutambua herufi za alfabeti ya Kiswahili.
- Kukariri sauti za alfabeti ya Kiswahili.
- Kuimba wimbo wa alfabeti ya Kiswahili
- Kutaja aina mbili kuu za sauti za Kiswahili.
- Kujibu maswali kuhusu alfabeti ya Kiswahili kwa usahihi.
Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
Maagizo
Kwa kutumia ubunifu na maneno yako mwenyewe, andika maelezo mafupi juu ya somo hili kwenye kitabu chako cha mazoezi unapoendelea kusoma na kisha uwasilishe maelezo yako kwa mwalimu wako wa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha uhakiki na maoni yanayofaa.
Msamiati
Shughuli: Activity
Alfabeti: Alphabet
Andika: Write
Sauti: Sound
Sehemu: A part of
Herufi: Letter of the alphabet
Gawika: Broken
Kwa utaratibu maalum: In a special order
Jumla ya: A total of
Jumuisha: Consists of
Changamano: Complex
Shughuli: Activity
Husisha: Associate/relate
Dhihirishwa – Manifested / shown
Kariri: Memorize
Ubunifu: Creativity
Alama: Mark.
Shughuli 1: Alfabeti ya Kiswahili
Sauti ni sehemu ndogo kabisa ya neno ambayo haiwezi kugawika zaidi, na hudhihirishwa kwa mlio unaotokana na tamko.
- Sauti huandikwa kwa kutumia alama zinazoitwa herufi.
- Jumla ya herufi za lugha ambazo zimepangwa kwa utaratibu maalum uliokubaliwa huitwa Alfabeti.
- Alfabeti ya Kiswahili inajumuisha herufi thelathini.
- Kila herufi ya alfabeti ya Kiswahili inahusishwa na sauti moja tu.
Shughuli 2: Kukariri kwa alfabeti ya Kiswahili
Jifunze wimbo wa alfabeti ufuatao kisha uutumie kuandaa ngoma maalum ya kuburudisha wanafunzi wengine darasani.
Shughuli 3: Alfabeti kamili ya Kiswahili
Andika alfabeti ya Kiswahili katika kitabu chako cha mazoezi.
a
b
ch
d
dh
e
f
g
gh
h
i
j
k
l
m
n
ng’
ny
o
p
r
s
sh
t
th
u
v
w
y
z
Kumbuka: Alfabeti ya Kiswahili haina herufi c, q, na x.