Shabaha
- Kutaja irabu zote za Kiswahili.
- Kuimba wimbo wa irabu za Kiswahili.
- Kutaja na kuandika alfabeti ya Kiswahili kwa mpangilio sahili.
- Kujibu maswali kuhusu sauti za Kiswahili kwa usahihi.
Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
Kudurusu
- Sauti ni kipashio kidogo kabisa cha neno ambacho kinaweza kutamkwa, lakini hakiwezi kugawika zaidi.
- Herufi ni alama ambazo zinatumiwa kuandika sauti.
- Alfabeti ni jumla ya herufi za lugha ambazo zimepangwa kwa utaratibu maalum.
- Alfabeti ya Kiswahili ina herufi thelathini.
- Kila herufi ya alfabeti ya Kiswahili inahusishwa na sauti moja tu.
- Alfabeti ya Kiswahili haina herufi c, q, na x.
- Aina mbili kuu za sauti katika alfabeti ya Kiswahili ni irabu na konsonanti.
- Alfabeti kamili ya Kiswahili ni:
A, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, l, m, n, ng’, ny, o, p, r, s, sh, t, th, u, v, w, y, z.
Maagizo
Kwa kutumia ubunifu na maneno yako mwenyewe, andika maelezo mafupi juu ya somo hili kwenye kitabu chako cha mazoezi unapoendelea kusoma na kisha uwasilishe maelezo yako kwa mwalimu wako wa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha uhakiki na maoni yanayofaa.
Msamiati
Alama: Mark.
Alfabeti: Alphabet
Gawika: Broken
Herufi: Letter of the alphabet
Husisha: Associate/relate
Irabu/vokali/Voweli: Vowel
Jumla ya: A total of
Kariri: Memorize
Kipashio: A piece/part
Konsonanti: Consonant
Kwa utaratibu maalum: In a special order
Makundi: Groups
Rejelea: Refer
Sauti: Sound
Shughuli: Activity
Ubunifu: Creativity
Shughuli 1: Voweli za Kiswahili
Irabu ni aina ya sauti katika alfabeti ya Kiswahili.
- Irabu za Kiswahili hurejelewa kwa majina mengine kama vokali na voweli.
- Kuna jumla ya irabu tano (5) katika alfabeti ya Kiswahili.
- Irabu za Kiswahili huandikwa kwa herufi zifuatazo:
a
e
i
o
u
Shughuli 2: Kukariri Voweli za Kiswahili
Imba wimbo ufuatao kwa pamoja ili kukariri voweli za Kiswahili.