Shabaha
- Kueleza maana ya silabi.
- Kutaja sifa bainifu za silabi katika lugha ya Kiswahili.
- Kueleza tofauti kati ya silabi na sauti.
- Kueleza jinsi ya kutambua silabi katika neno.
- Kueleza umuhimu wa silabi.
Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
Kudurusu
- Sauti ni sehemu ndogo kabisa ya neno ambayo haiwezi kugawika zaidi, na hudhihirishwa kwa mlio unaotokana na tamko.
- Sauti mbili kuu za lugha ya Kiswahili ni irabu na konsonanti.
- Herufi ni alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha ya Kiswahili.
- Sauti huandikwa kwa kutumia herufi ndogo pekee.
- Alama za mshazari zinapowekwa pande zote mbili za herufi katika andiko huonyesha kuwa andiko hilo ni la sauti.
Maagizo
Kwa kutumia ubunifu na maneno yako mwenyewe, andika maelezo mafupi juu ya somo hili kwenye kitabu chako cha mazoezi unapoendelea kusoma na kisha uwasilishe maelezo yako kwa mwalimu wako wa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha uhakiki na maoni yanayofaa.
Msamiati
Alama ya kijistari: Hyphen
Andika: Write
Dhihirisha: Manifest/Show
Fungu: Part
Jumuisha: Comprise/Include
Kati ya: Between
Kopa: Borrow
Lugha: Language
Maana: Meaning
Mchanganyiko: A combination
Moja: One
Muhimu: Important
Neno: Word
Onyesha: Show
Pigo la sauti: A sound beat
Rejelea: Refer
Sauti: Sound
Sehemu: A part of
Sifa bainifu: Characteristic features
Silabi: Syllable
Tahajia: Spelling
Tambua: Recognize/Realize
Tamka: Pronounce
Tenganisha: Separate
Tumia: Use
Unganisha: Connect.
Shughuli 1: Maana ya silabi
- Silabi ni sehemu ya neno ambayo inatamkika kama tamko moja la sauti. Hurejelewa kwa namna nyingine kama pigo la sauti katika neno.
- Silabi za Kiswahili zinaweza kuhesabika.
- Njia moja ya kutambua silabi katika neno fulani ni kwa kuhusisha kila sauti ya kipekee inayotamkwa na pigo moja, ifuatavyo:
Neno
Silabi katika neno
Kuhesabu silabi
Jumla ya mapigo
Kiswahili
ki-swa-hi-li
4
silabi
si-la-bi
3
sauti
sa-u-ti
3
kinatamkwa
ki-na-ta-m-kwa
5
mchanganyiko
m-cha-nga-nyi-ko
5
konsonanti
ko-nso-na-nti
4
Kumbuka: Alama ya kijistari, hutumiwa kutenganisha silabi za neno.
Shughuli 2: Sifa bainifu za silabi katika lugha ya Kiswahili
Katika lugha ya Kiswahili silabi:
- ni sehemu au kitengo kimoja cha neno.
- inatamkwa kama tamko moja lisilokatika la sauti
- inaweza kujumuisha mchanganyiko wa vokali na konsonanti.
- inaweza kujumuisha herufi moja au zaidi ya alfabeti ya Kiswahili.
- Ina sauti moja tu
Jedwali lifuatalo linajumuisha vielelezo vya sifa za silabi:
Herufi
Silabi
Tamko
e
=
e
m
=
m
m + e
=
me
m + b + e
=
mbe
m + b + w + e
=
mbwe
Shughuli 3: Umuhimu wa silabi katika lugha ya Kiswahili
- Silabi hutumiwa katika uundaji wa maneno ya Kiswahili.
- Silabi hurahisisha:
- kutamkwa kwa maneno.
- kusomwa kwa maneno.
- kuandikwa kwa maneno.
- kutahajia maneno.