Shabaha
- Kueleza dhima ya International Phonetic Alphabet (IPA)
- Kutambua shirika linalodhibiti IPA
- Kueleza mahali pa kupata IPA mtandaoni
- Kueleza jinsi ya kutumia IPA kubaini sauti za maneno.
Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
Kudurusu
- Sauti ni sehemu ndogo kabisa ya neno ambayo haiwezi kugawika zaidi, na hudhihirishwa kwa mlio unaotokana na tamko.
- Silabi ni pigo la sauti.
- Neno ni kitengo kidogo cha lugha. Huundwa kwa silabi ambazo zimefungamanishwa na kuleta maana.
Maagizo
Kwa kutumia ubunifu na maneno yako mwenyewe, andika maelezo mafupi juu ya somo hili kwenye kitabu chako cha mazoezi unapoendelea kusoma na kisha uwasilishe maelezo yako kwa mwalimu wako wa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha uhakiki na maoni yanayofaa.
Msamiati
Agizo: Instruction
Alfabeti ya Kifonetiki: Phonetic Alphabet
Ainisha: Classify
Baini: Find out/Establish
Bofya: Click
Chapisha: Publish
Dhibiti: Control
Dhima: Function
Geni: Alien/New
Julikana: Known
Jumuishi: Integrated
Kiungo: Link
Konsonanti: Consonant
Maalum: Special
Maana: Meaning
Makini: Carefully/attentively
Maoni: Comments/Feedback
Matamshi: Pronunciation
Mfumo: System
Miongoni: Among
Mtandao: Internet
Neno: Word
Orodha: List
Rahisi: Easy
Rejelea: Refer
Sahihi: Correct
Sanifisha: Standardize
Sarufi: Grammar
Sauti: Sound
Sawa: Same/Equivalent
Sehemu: A part of
Shirika: Organization
Shughuli: Activity
Silabi: Syllable
Tafsiri: Translate
Tahajia: Spelling
Tambua: Recognize/Realize
Tamka: Pronounce
Tegemea: Depend on
Tembelea: Visit
Tofauti: Different
Ubunifu: Creativity
Uhakiki: Review
Ulimwengu: The Word
Voweli: Vowel
Wakilisha: Represent
Wezesha: Enable
Zaidi: More
Zingatia: Consider/Focus on.
Shughuli 1: Dhima ya International Phonetic Alphabet (IPA)
International Phonetic Alphabet (IPA) ni mfumo maalum unaowezesha watu kote ulimwenguni kutambua sauti mbali mbali zinazotumika katika matamshi kwa urahisi, na kuzitamka kwa usahihi na kwa njia sawa.
Katika alfabeti hii, sauti za kifonetiki zinawakilishwa na ishara maalum ambazo zimesanifishwa.
Kila sauti tofauti ina ishara yake maalum. Ishara sahihi hutambuliwa kwa kusikiliza sauti inapotamkwa kwa makini. Haitegemei tahajia ya neno.
Sauti zinazopatikana katika lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa sauti ambazo zimeorodheshwa katika International Phonetic Alphabet.
Shughuli 2: Uzalishaji na udhibiti wa International Phonetic Alphabet
Mambo yanayozingatiwa katika fonetiki yanajumuisha kuzalisha, kutamka, kusambaza, kupokea na kuainisha sauti. Shirika ambalo lina jukumu la kuandaa, kuchapisha, na kusimamia alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa ni International Phonetic Association.
Kwa habari zaidi kuhusu International Phonetic Association na kazi zake, bofya kiungo kifuatacho:
Shughuli 3: Orodha kamili ya sauti katika International Phonetic Alphabet (IPA)
Alfabeti ya kifonetiki imechapishwa katika sehemu mbili, ambazo ni konsonanti na voweli.
- Bofya kiungo kifuatacho ili kuona sauti zote za konsonanti ambazo zimeorodheshwa katika International Phonetic Alphabet.
- Bofya kiungo kifuatacho ili kuona sauti zote za voweli ambazo zimeorodheshwa katika International Phonetic Alphabet.
Shughuli 4: Jinsi ya kutumia International Phonetic Alphabet kubaini sauti za maneno
Unapokutana na neno geni ambalo maana na matamshi yake hayajulikani, unaweza:
- kwanza kurejelea kamusi jumuishi ya lugha husika ili kubaini maana ya neno hilo na ishara zake za kifonetiki, halafu
- ukirejelea International Phonetic Alphabet (IPA), utafsiri ishara za neno ili kupata sauti na hivyo matamshi yake sahihi.