Description
Kumbuka: Katika mada hii tutazingatia shadda katika neno.
Shughuli 1: Aina tofauti za silabi katika neno kwa kuzingatia shadda
Kwa kuzingatia shadda, neno moja linaweza kuwa na hadi aina tatu tofauti za silabi zifuatazo:
- Silabi yenye mkazo wa msingi
- Silabi yenye mkazo wa pili
- Silabi zisizo na mkazo.
Shughuli 2: Silabi zenye mkazo wa msingi
Kwa kawaida kuna silabi moja haswa kwa kila neno yenye kiwango cha juu zaidi cha mkazo kuliko zingine. Silabi hii inaweza kurejelewa kuwa yenye mkazo wa msingi.
Silabi yenye mkazo wa msingi inaweza kuathiri maana ya maneno.
Ili kuonyesha mkazo wa msingi katika neno, alama ya shadda huwekwa pale juu punde tu kabla ya silabi inayopokea mkazo wa msingi, kama inavyoonyeshwa katika mifano ifuatayo:
[saˈfari]
[ˈwatu]
[viˈtabu]
Shughuli 3: Silabi zenye mkazo wa pili
Aina hii ya silabi ina mkazo fulani lakini wenye kiwango kidogo ukilinganishwa na ule wa silabi yenye mkazo wa msingi. Neno moja linaweza kuwa na silabi zaidi ya moja zenye mkazo wa pili.
Isipokuwa silabi iliyo na mkazo wa msingi, silabi zingine zozote zinazosisitizwa husemekana kuwa na mkazo wa pili.
Ili kuonyesha mkazo wa pili katika neno, alama ya shadda huwekwa pale chini, punde tu kabla ya silabi inayopokea mkazo.
Zoezi
Aina na za shadda katika neno
Reviews
There are no reviews yet.