Description
Shughuli 1: Umbo la alama ya shadda
Alama ya shadda in mojawapo ya alama ambazo zimeorodheshwa katika Alfabeti ya Kifonetiki ya Kimataifa (International Phonetic Alphabet, IPA).
Alama ya mkazo inawakilishwa na kijistari kifupi cha wima [‘].
Shughuli 2: Tofauti kati ya alama za shadda, ritifaa, na koma
Sifa za alama hizo tatu, ikijumuisha umbo na dhima zao, zimeangaziwa katika kielelezo kifuatacho. Tambua tofauti kati ya alama hizo tatu kwa kulinganisha sifa zao.

- Alama ya shadda ni tofauti na alama ya ritifaa na ile ya koma katika:
- Umbo: Kwa kawaida shadda huonyeshwa kwa kijistari kifupi cha wima.
- Uamilifu: Alama ya shadda ni ya aina ya kifonetiki, ilhali zile za ritifaa/apostrofi na koma ni alama za uakifishaji.
Shughuli 3: Nafasi ya alama ya shadda/mkazo katika neno
Alama ya shadda huonyesha silabi inayopokea mkazo zaidi katika neno. Wakati ambapo matamshi ya neno yanaonyeshwa, alama ya shadda huwekwa punde tu kabla ya silabi inayopokea mkazo.
[saˈfari]
[maˈziwa]
[ˈwatu]
[ˈsisi]
[viˈtabu]
[mˈkoba]
Unapoiona alama hii ina maana kwamba unafaa kuweka mkazo zaidi kwenye silabi inayokuja mara tu baada ya alama hiyo. Unaweza, kwa mfano, kuitamka silabi hiyo kwa nguvu zaidi au kwa sauti ya juu zaidi, au hata kwa muda mrefu zaidi ili kuwasilisha maana inayokusudiwa.
Reviews
There are no reviews yet.