Description
Shughuli 1: Jinsi ambavyo Konsonanti zimeainishwa katika makundi
Jedwali lifuatalo linaonyesha, kwa ufupi, jinsi konsonanti zimeainishwa kwa kuzingatia aina tatu za vigezo (mahali pa kutamkia, mtetemo wa nyuzi za sauti, jinsi hewa inavyozuiliwa).

Shughuli 2: Wimbo kuhusu mahali pa kutamkia konsonanti za Kiswahili
Kariri wimbo ufuatao ili kukumbuka kwa urahisi mahali pa kutamkia konsonanti za Kiswahili. Imba wimbo huku ukifuatilia sauti tofauti katika safu-wima kwa mpangilio wa kushuka chini.
Mahali pa kutamkia konsonanti za Kiswahili
Konsonanti za midomoni; /p/, /b/, /m/, /w/
Midomo meno; /f/, /v/
Meno ulimi; /th/, /dh/
Konsonanti za ufizini; /s/, /z/, /t/, /d/, /n/, /l/, /r/
Ufizi kaakaa gumu; /ch/
Kaakaa gumu; /sh/, /j/, /ny/, /y/
Kaakaa laini; /gh/, /k/, /g/, /ng’/
Na koromeo; /h/
Shughuli 3: Sauti likwidi
Sauti likwidi ni sauti ambazo hutamkwa wakati ala za sauti zinapokaribiana na kutatiza hewa kwa namna maalum, huku hewa ikiendelea kupita. Aina mbili za sauti likwidi ni:
- kitambaza /l/
- kimadende /r/.
Shughuli 4: Wimbo wa konsonanti sighuna za Kiswahili
Kariri wimbo ufuatao ili kukumbuka kwa urahisi konsonanti sighuna za Kiswahili.
Konsonanti sighuna za Kiswahili
Konsonanti siguna ni tisa
Vipasuo vitatu; /p/, /t/, /k/
Kipasuo kwamizo kimoja; /ch/
Za mwisho tano ni vikwamizo /f/, /th/, /s/, /sh/, /h/.
Reviews
There are no reviews yet.