Description
Shughuli 1: Maana ya vitenzi
- Vitenzi ni maneno yanayorejelea vitendo.
- Vitenzi ni mojawapo ya aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili.
Shughuli 2: Dhima za vitenzi
Vitenzi vina uamilifu tofauti wa kisarufi. Zifuatazo ni baadhi ya dhima za vitenzi.
a)Â Â Vitenzi huashiria vitendo, matukio, au hali za kuwa kwa vitu

Watoto wanakimbia.
The children are running.

Kunanyesha
It is raining.

Hawa ni watoto.
These are children.
b) Vitenzi huwezesha uundaji wa vishazi vinavyoleta maana
- Kishazi ni fungu la maneno lenye kiima kimoja na kiarifa kimoja. Wingi wa kishazi ni vishazi.
- Kishazi huru huhitaji tu kiima kimoja na kiarifu kimoja ili kuleta maana.
- Sentensi inaweza kuundwa kwa kutumia kishazi kimoja, au vishazi zaidi ya moja.
- Mtoto analala. (The baby is sleeping).
- Maria atanunua kitabu kesho. (Maria will buy a book tomorrow).
- Mwashi alijenga nyumba tatu. (The mason built three houses).
- Watoto walifurahii walipokuwa wakicheza. (The children were happy when they were playing).
c) Vitenzi huwezesha uwasilishaji wa nyakati na vipengele vinavyohusiana na wakati.
Vitenzi vinaweza kurekebishwa kwa kutumia mbinu kama vile unyambulishaji, uambatanishaji, au kwa kuviongezea vitenzi visaidizi, ili kuwasilisha
- nyakati tofauti
- vipengele vinavyohusiana na wakati kama vile hali ya kukamilika kwa kitendo, muda wa kitendo, au kurudia kwa kitendo.
Nyakati / Hali
Mifano katika sentensi
Nyakati tofauti
Mama anapika ugali. (Mother is cooking ugali.)
Mama alipika ugali. (Mother cooked ugali.)
Mama atapika ugali. (Mother will cook ugali.)
Hali ya mazoea
Mama hupika ugali jioni. (Mother cooks ugali in the evening.)
Hali timilifu
Mama amepika ugali. (Mother has cooked ugali.)
d) Vitenzi huwezesha uwasilishaji wa dhamira na mtazamo wa msemaji/mwaandishi
Vitenzi vinaweza kutumiwa kuwasilisha dhana mbalimbali kama vile; pendekezo, uwezo, wajibu, ushauri, mwaliko, ombi, hitimisho, agizo, uwezekano, ulazima, ruhusa, na kutoidhini.
Alama za uakifishaji hutumiwa katika maandishi kuwashilisha baadhi ya dhana hizi.
Dhana
Mifano katika sentensi
Ombi
Ninaweza kuimba nyimbo mbili? (May I sing two songs?)
Agizo
Imba! (Sing!)
Uwezo
Ninaweza kuandika vizuri. (I can write well.)
Wajibu
Unapaswa kuhudhuria mkutano. (You should attend the meeting.)
Ruhusa
Unaweza kwenda nyumbani. (You can go home).
e) Vitenzi huwezesha makubaliano ya kisarufi.
Katika lugha ya Kiswahili, ngeli za nomino zilizo katika sentensi fulani huathiri miundo ya aina zingine za maneno ambayo yanahusiana nazo, kama vile; vitenzi, vivumishi, na vimilikishi.
Kwa kuchukua viambishi tofauti kama vile ambavyo vinaonyesha ngeli za nomino pamoja na idadi, vitenzi huwezesha uundaji wa sentensi zilizo sahihi kisarufi.
- Mwanafunzi alisoma kitabu. (The student read a book.)
- Wanyama wanalala. (The animals are sleeping.)
- Kiti kilivunjika. (The chair broke.)
- Mti una matunda. (The tree has fruits.)
- Nguo zimekauka. (The clothes are dry.)
Reviews
There are no reviews yet.